Msanii wa filamu nchini na Miss
Tanzania 2006, Wema Sepetu, mchana huu amepandishwa kizimbani kwenye
mahamaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Akisomewa mashtaka na wakili wa serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu
Mkazi Thomas Simba imeelezwa kuwa msanii huyo alikutwa na kiwango kidogo
cha dwa za kulevya aina ya bangi
Wakili Nassoro Katuga amesema mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa Wema Sepetu
mnamo tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2017 katika eneo la Kunduchi Ununio
watuhumiwa watatu akiwemo Wema Sepetu walitenda kosa hilo kinyume na
kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa ya kulevya kifungu cha
17 (1) (a) cha makosa hayo.
Msanii huyo na wenzake wameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 na
wadhamini wawili na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 22 Februari 2017
itakapotajwa tena na kwamba bado uchunguzi unaendelea.
Post a Comment