Mfalme wa Rwenzururu Wesley Mumbere
Wabunge kutoka
Kasese, magharibi mwa Uganda , wanasema wamezuiliwa na vyombo vya
usalama kukutana na mfalme wa Rwenzururu, Wesley Mumbere, licha ya
mfalme huyo kuachiliwa kwa dhamana.
Wabunge hao ambao wote ni
kutoka chama cha upinzani cha FDC, wanasema kuwa ni kama ambaye mkubwa
wao yuko katika kizuizi cha nyumbani.Kulingana na mwandishi wetu wa Kampala Siraj Kalyango wabunge wanne kutoka Kasese, Winfred Kiiza, Harlod Muhindi, William Nzoghu na Robert Muhindo wamelalamika kuwa mfalme wao anadhalilishwa.
Mfalme Mumbere amekuwa korokoroni tangu mwaka jana kwa sababu zinazohusika na uchochezi.
- Mfalme wa Uganda kupata mpishi Jela
- Walinzi wa mfalme waliwaua polisi 16 Uganda
- Mfalme akamatwa kwa kuchochea ghasia Uganda
- Mfalme wa Rwenzururu afunguliwa mashtaka ya Ugaidi
Febuari 6 mwaka huu mahakama ya juu ya mjini Jinja ilimuachilia Mumbere kwa dhamana ya polisi ya shilling za Uganda millioni 100 sawa na dola za Marekani 27,894, na wabunge hao ndio wadhamini wake.
Pia mfalme huyo aliamriwa kuwa kila baada ya muda fulani itambidi kurudi mahakamani.
Jumatatu anatakiwa kufanya hivyo na sasa yuko nyumbani kwake hapa mjini Kampala.
Post a Comment