0

 
Mwenyekiti  wa  Uwt  wilaya  Masasi  Jubulei  Sowani  akimkabidhi  Jane  Joseph  Sabuni  mgonjwa  aliyelazwa  wordi ya  wanawawake  na  watoto katika  hospitali  ya Ndanda  wakati  walipokwenda kusaidia  vifaa  mbalimbali  ikiwa  ni  moja ya kuhazimisha miaka  40  ya  chama  cha  mapinduzi

Na  Fadhila  Milanzi  Masasi
Upungufu  wa  damu  katika  Hospitali ya   Ndanda  mkoani  Mtwara  imeelezwa  kuwa  ni  moja  ya  sababu  inayochangia  ongezeko  la  vifo  vya  mama wajawazito  na  watoto

Hayo  yameelezwa  na  muuguzi  wa  wordi  ya  mama  wajawazito  na   watoto  Renfrida  Hokororo  wakati alipokuwa  anazungumza  na uongozi  wa  umoja  wa wanawake Ccm  Wilaya  ya  Masasi  wakati  walipokwenda  kutoa  misaada  ya  vifaa  mbalimbali  katika wordi  hiyo.

Renfrida  alisema  tatizo la  damu  kwa  mama wajawazito  na  watoto  katika  hospitali  hiyo   ni  kubwa  hivyo  ni  vyema  wanawake na jamii   kwa  ujumla ikaona  umuhimu   wa  kuchangia  damu  ili  kuokoa  maisha  ya  wanawake  na  watoto

Alisema kuwa  katika  kipindi  cha  mwenzi  januari  wanawake  tisa  walilazwa katika  wordi  hiyo  lakini  mama  mmoja  alipoteza  maisha  baada ya  kukosa  damu  kutokana  na  banki  ya  damu  kukosa  damu ya  group  lake.

 ‘Kwa  niaba  ya uongozi wa  hospitali  ya natoa  shukrani kwa msaada mulioleta lakini  niwaombe wanawake mwenzangu kuangalia uwezekano  wa  kuchangia  damu  kwa ajili  ya kuokoa  maisha ya  watoto wetu  na  wanawake wezetu  wanaolazwa katika  wordi  hizi’  alisema  Hokororo.

Velonica Mmole muunguzi  mkunga  alisema kuwa kitendo kilichofanywa  na  wanawake  wa  jumuhia ya  wanawake wa  chama  cha  mapinduzi  inastaili  kuigwa kwani kimeonyesha  ualisimia  wa  matendo  ya  wanawake  ya  kuhurumiana

Mwenyekiti  wa  jumuhia  ya  wanawake wilaya  Masasi (UWT)Jibulei Sowani  ameiomba  jamii  kuchangia   damu  ili  kuokoa  maisha  ya  wanawake  na  watoto  ambao  ni  taifa  la kesho

Alisema  ili kutengeneza  taifa  zuri  la  kesho  hakuna  budi kila  mmoja  kuona  umuhimu  wa  kuwasaidia  watoto  na  wanawake  wajawazito  kwa  kuchangia  damu  ili  wajifungue  salama

 Sowani aliongeza  kuwa wanawake  wilayani  masasi  wameguswa  na tatizo  hilo  hivyo  watajipanga  na  kuangalia uwezekano  wa kuchangia  damu  kila inapohitajika  

Aidha viongozi na wananchama wa umoja wanawake  wa chama cha mapinduzi  katika  madhimisho ya kuzaliwa  chma  hicho walifanya zoezi la  usafi na kutoa msaada wa sabuni kwa wagonjwa hasa wakina mama na watoto   linapojitokeza

Post a Comment

 
Top