Shughuli za kukarabati
zinaendelea kwenye jengo ya bunge baada ya upepo mkali kung’oa sehemu za
paa la jengo hilo siku ya Jumanne jioni February 1 2017.

Tukio hilo lilisababisha kusitishwa ghafla kwa vikao vya bunge hilo la Ghana
baada ya mvua kuanza kuingia ndani ya jengo ambapo Wafanyakazi
walijaribu kukinga baadhi ya maeneo yaliyoachwa wazi kwa kukusanya maji
wakitumia ndoo.

BBC SWAHILI wameripoti kwamba jengo hilo la bunge lililopo kwenye mji mkuu wa Accra mara ya mwisho lilikarabatiwa miaka miwili iliyopita.
Post a Comment