Nyimbo zilizokuwa
zimepotea za mwanamuziki Bob Marley, ambazo zilipatikana kwenye chumba
cha chini cha hoteli mjini London baada ya zaidi ya miaka 40
zimetengenezwa upya tena.
Kanda hizo za hali ya juu ni zile Bob
Marley alirekodi moja kwa moja, wakati wa tamasha zake za miji ya London
na Paris kati ya mwaka 1974 na 1978.
Kanda hizo ni za nyimbo za No Woman No Cry, Jamming na Exodus.
Kwaza zilidhaniwa kuharibiwa kabisa kutokana na unyevu uliokuwa eneo kanda hizo zilipatikana.
Marley ambaye aliaga dunia mwaka 1981, angekuwa na umri wa miaka 72 hii leo.
Kanda
hizo zilipatikana kwenye hoteli ya Kensal Rise, kaskazini magharibi mwa
London, ambapo Bob Marley na bendi yake walikuwa wakiishi, wakifanya
tamasha zao barani Ulaya miaka ya sabini.
Kanda hizo ni kutoka kwa
tamasha zilizofanyika maeneo la Lyceum mjini London mwaka 1975, la
Hammersmith Odeon 1976, na la Rainbow mjini London mwaka 1977
Post a Comment