Marufuku ya Usafiri ya Trump: Marekani yataka kusimamishwa kwa muda
Kurejeshwa
tena kwa marufuku ya Rais Donald Trump kwa wahamiaji kutoka mataifa
saba ya kiislamu, itasababisha "fujo tena", mawakili kutoka Marekani
waonya.
Mawakili kutoka Washington na Minnesota, wanaiomba
mahakama kuu ya nchi hiyo huko San Francisco kuendelea kuzuilia amri
hiyo kuu kote nchini Marekani.
Wanaungwa mkono na kampuni za kiteknolojia, zinazosema kuwa
marufuku ya usafiri inahujumu biashara zao. Mawakili wa utawala wa
Trump, wanatarajia kujibu hilo baadaye Jumatatu.
Amri ya kusimamishwa kwa muda ilitolewa siku ya Ijumaa, na jaji mmoja wa serikali huko Seattle, Jijini Washington, ya kuahirisha agizo hilo kuu la Bw Trump, ya kuwazuia miaji kutoka mataifa hayo saba yenye waislamu wengi.
Watu walio na visa kutoka Iraq, Syria, Iran, Libya, Somalia, Sudan na Yemen, itaendelea kukubaliwa Marekani hadi pale kesi hiyo itakaposikizwa.
Amri hiyo ya Jaji ilipokelewa kwa hasira na Bwana Trump, ambaye alidai kuwa usalama wa taifa umo hatarini.
Ombi
la mahakama ya San Francisco tayari imepinga agizo la idara ya
mahakama, kutekeleza kizuizi cha muda, kinachopangiwa kuzikubalia
majimbo mawili kuwasilisha malalmishi yao inayosema kuwa marufuku hiyo
ni kinyume na sheria na hatari kwa wakaazi wao, biashara na hata vyuo
vikuu.
Mawakili
wao wameiambia mahakama hiyo ya rufaa kuwa, marufuku ya aina yoyote,
"itafufua madhara hayo, kutenganisha familia, kutatiza vyuo vyetu vikuu
na hata mtaala, na pia kutatiza sekta ya usafiri".
Mawakili hao
pia waliwasilisha taarifa za usalama wa taifa - inayowajumuisha mawaziri
wa zamani wa kigeni John Kerry na Madeleine Albright, na pia mkurugenzi
mkuu wa zamani wa idara ya ujasusi (CIA) Leon Panetta - ambaye
anaelezea marufuku hiyo ya usafiri kama isiyofaa, hatari na iliyojaa
hasara tupu.
Post a Comment