Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na watumishi wa
Sekretarieti ya Mkoa huo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya
uchunguzi gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa
Katibu
Tawala Mkoa wa Simiyu, Ndg.Jumanne Sagini akizungumza na watumishi wa
Sekretarieti ya Mkoa huo wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya awali ya
uchunguzi wa gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa.
Baadhi
ya Watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Katibu
Tawala Mkoa huo, Ndg.Jumanne Sagini wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya
awali ya uchunguzi wa gharama za ujenzi wa Hospitali ya Mkoa.
Na Stella Kalinga
Mhandisi wa Ujenzi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Simiyu, Deusdedit Mshuga amesimamishwa kazi kwa kukabiliwa na mashtaka matatu.
Akizungumza
na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu,
Ndg. Jumanne Sagini amesema Mhandisi huyo anashtakiwa kwa kushindwa
kutekeleza majukumu aliyopewa kwa kiwango cha kuridhisha.
Amesema
akiwa mtumishi wa umma kinyume na kipengele cha 8 cha sehemu"A" ya
jedwali la kwanza la kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali
Na.168/2003; mtumishi huyo alishindwa kuandaa makadirio ya gharama za
ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa yenye uhalisia.
Aidha
, Aliandaa makadirio ya Tsh46,106,456,000 yaliyosomwa mbele ya Mhe.
Rais tarehe 11 Januari,2017 ambayo ni ya juu kuliko uhalisia.
Shtaka
la pili linalomkabili ni kufanya uzembe mkubwa wakati wa utekelezaji wa
majukumu ya kazi iliyopewa kinyume na kipengele cha 13 cha sehemu "A"
ya jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma,Tangazo la Serikali
na 168/2003;
Alitaja
(1) kuandaa makadirio ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa
Tshs.46,106,456,000 hali iliyosababisha Mhe Rais kusomewa taarifa ya
gharama zisizo na uhalisia na(2) Kuandaa michoro ya taswira (3
D)isiyoendana na michoro halisi ya Hospitali ya Mkoa iliyooneshwa mbele
ya Mhe.Rais
Shtaka
la tatu ni kufanya kazi kwa kukiuka maadili ya taaluma yake wakati wa
utekelezaji ya kazi aliyopewa kinyume na kipengele cha 14 cha Sehemu "A"
ya Jedwali la kwanza la Kanuni za Utumishi wa Umma, Tangazo la Serikali
Na.168/2003:- kwa (1) Kuandaa makadirio ya shilingi 46,106,456,000 ya
gharama za ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa bila kuzingatia mita za
mraba za eneo, michoro na kusababisha gharama kubwa zisizo na uhalisia
(2)
Kuandaa makadirio ya shilingi 3,009,640,000 yasiyo na uhalisia ili
kugharamia ujenzi wa majengo ya msingi kuwezesha Hospitali kuwa
"functional" kwa kupiga simu Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida.
Katibu
Tawala wa Mkoa, Ndg..Jumanne Sagini ametoa wito kwa watumishi wa Umma
mkoani humo kutekeleza majukumu waliyopewa kwa bidii, weledi na uadilifu
ili kuepuka makosa ambayo husababisha watumishi kuchukuliwa hatua za
kinidhamu.
“Nikiwa
kama mwajiri nimesikitishwa na kufadhaishwa na wataalam walioajiriwa
ngazi ya mkoa kuishauri Sekretarieti ya Mkoa na kuzisimamia Mamlaka za
Serikali za Mitaa na kuzishauri kitaalam, kutenda matendo
yanayodhihirisha upungufu wa weledi, kushindwa kutekeleza majukumu na
uzembe mkubwa” alisema.
Naye
Mkuu wa Mkoa huo,Mhe. Anthony Mtaka amesema gharama zilizowasilishwa
awali na wataalam hazikuwa na mchanganuo toshelevu na makisio hayakuwa
na uhalisia, hivyo amemwomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, kwa taarifa za upotoshaji
zilizotolewa na wataalam wakati wa ziara yake Mkoani humo.
“....kuna
vitu vingine vilivyopachikwa kwenye ramani, wenye taaluma yao
walipokutana ili kujustify hiyo bilioni 46.1 walishindwa kujustify
kwenye ramani, kwa hiyo hatukuwa na uhalisia; baada ya mapitio ya kazi
zote ilionekana Hospitali ya Mkoa wa Simiyu inaweza kujengwa kwa gharama
ya bilioni 11.4 mule mule alimosema Rais” alisema Mtaka.
Makadirio
ya awali ya Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa yalikuwa ni shilingi bilioni
46.1 na gharama hii haikukubaliwa na Mhe.Rais na badala yake akaagiza
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kutembelea TBA Makao Makuu, ili
kujifunza na kuona jinsi walivyoweza kujenga majengo ya hosteli ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam kwa gharama ndogo ya shilingi bilioni 10 na
akaahidi kutoa bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
Post a Comment