Naibu waziri wa
afya wa Tanzania, Hamis Kigwangalla ameendelea kusisitiza azma yake ya
kuchapisha orodha ya majina ya watu anaowashutumu kujihusisha na mapenzi
ya jinsia moja
Katika mjadala mkali ulioendelea kwenye mtandao wa
twitter na watumiaji wengine, Kigwangalla ametetea uamuzi wake huo kwa
kusema watu hawa si tu wanajihusisha na vitendo visivyokubalika katika
jamii. bali pia wanauza ngono kwa njia ya mtandao na kuhamasisha vitendo
vya mapenzi ya jinsia moja vyote vikiwa kinyume na sheria za nchi"Kuna watu wanadhani vita dhidi ya ushoga ni ya mzaha, ni vita kubwa na tutaishinda. Mtandao ni mrefu na nitaendesha operation kamata kamata," aliandika Kigwangala katika Twitter wiki iliyopita
- Wapenzi 3 wa jinsia moja watakiwa kuripoti polisi Tanzania
- Tanzania yasimamisha huduma za vituo 40 vya afya
Aliendelea kwa kutoa mfano kwamba katika vijiji vya mji anaotoka Nzega, katikati Magharibi mwa Tanzania, hakuna kabisa vitendo vya ushoga.
Wengi katika twitter walimshutumu Kigwangalla kwa kuendesha kampeni ya chuki dhidi ya kundi hilo la mashoga huku yeye akijibu, "natimiza wajibu wangu kama kiongozi msimamizi wa sheria na sera za nchi yetu."
Hatua hii ya Kigwangalla inaambatana na uamuzi wa serikali kuvifungia vituo vipatavyo 40 vya afya ambavyo vilikuwa vikitoa huduma za UKIMWI ikiwa ni pamoja na kwa makundi ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja
Nchini Tanzania, mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria na adhabu yake inaweza kuwa hata miaka 30 jela.BBC
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.