Leo Februari 21, 2017 Mahakama Kuu imeamuru Mwenyekiti wa CHADEMA,
Freeman Mbowe asikamatwe hadi maombi yake kutokamatwa yataposikilizwa
siku ya Ijumaa.
Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni tarehe 10 mwezi huu
alifungua kesi ya Kikatiba dhidi ya RC Paul Makonda, Kamanda Simon
Sirro.
Aidha Mahakama imewaushauri upande wa mlalamikaji kurekebisha hati ya mashtaka kisha wairudishe tena siku ya Jumatatu.
Siku ya jana Mawakili wa Mbowe waliweka pingamizi la kutokamatwa kwa
kiongozi huyo lakini kabla taarifa hazijalifikia Jeshi la Polisi, Mbunge
huyo wa Hai akatiwa nguvuni
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.