Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka
mabalozi wa Tanzania katika nchi mbalimbali kuhakikisha wanatumia uwakilishi
wao kutafuta wawekezaji watakaokuja kuwekeza katika sekta ya viwanda nchini.
Amesema mkakati wa serikali ni kuimarisha uchumi hadi wa kati kupitia
sekta ya viwanda, hivyo jukumu la mabalozi hao ni kuhakikisha jambo hilo
linafanikiwa.
Waziri
mkuu ametoa kauli hiyo alipokutana na mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania katika
nchi za nje akiwemo balozi dk. emmanuel nchini (brazil), balozi elizabeth
kiondo (uturuki), balozi george madafa (italy), balozi james msekela
(uswisi),balozi samuel shelukindo (ufaransa), balozi paul mella (drc), balozi
mbelwa kairuki (china).
Pia waziri mkuu amewataka mabalozi hao kutumia
uwakilishi wao katika nchi hizo kwa kuhakikisha wanatangaza vivutio vya utalii
vilivyopo nchini ili kuongeza idadi ya watalii wanaokuja Tanzania.
aidha,
waziri mkuu amewataka mabalozi hao kulinda maslahi ya taifa katika nchi
hizo ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na mataifa
hayo.
katika
hatua nyingine, waziri mkuu amewataka mabalozi hao
kuhakikisha wanawatambua watanzania wanaoishi katika mataifa hayo na
kushirikiana nao katika kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini.
kwa
upande wake balozi mella ambaye amezungumza kwa niaba ya mabozi wenzake
alimuhakikishia waziri mkuu kwamba watakwenda kutekeleza wajibu wao ipasavyo.
Post a Comment