0
Kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI imeitaka serikali kufungia uzalishaji na uuzaji wa bombe za bei rahisi maarufu kama viroba kutokanana kuwepo kwa uhusiano mkubwa na ongezeko la tabia hatarishi zinazochangia ongezeko la vijana kuingia katika matumizi  ya dawa za kulevya.

Akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati ya kudumu ya bunge ya masuala ya UKIMWI kwa mwaka 2016/17, makamu mwenyekiti wa kamati Mhe. Jasmine Bunga amesema hali hiyo inaathiri ufanisi wa nguvu kazi na kuhatarisha taifa, ambapo ametaka viongozi wa wakuu wa nchi kutoa kauli ili kuhamasisha jamii kuunga mkono katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

Wakichangia maoni kuhusu taarifa za shughuli za kamati za bunge za maswala ya UKIMWI na kamati ya huduma za maendeleo ya jamii baadhi ya wabunge wameitaka kukamata wauzaji wa dawa za kulevya na waathirika wapelekwe katika matibabu badala ya rumande, huku wengine wakitaka serikali kuboresha matibabu kwa kuongeza dawa ili wananchi waweze kupata huduma kwa wakati.

Awali akiwasilisha taarifa ya shughuli za kamati ya kudumu ya bunge ya huduma za maendeleo ya jamii, mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe Peter Selukamba amesema kamati hiyo imebaini hali ya upatikanaji wa dawa katika maeneo mengi si wa kuridhisha kutoka sababu mbalimbali ikiwemo bohari kuu ya dawa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kuagiza dawa toka nje ya kutokana na madeni mengi inayozidai halmashauri nyingi nchini.

Post a Comment

 
Top