0
Idadi ya watu waliofariki dunia katika ajali iliyotokea katika eneo la Mwika Mawanjeni mkoani Kilimanjaro imeongezeka na kufikia wanane huku jeshi la polisi likitangaza kumsaka Dereva wa Fuso James John aliyekimbia baada ya ajali
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro kamishna masaidizi mwandamizi wa polisi Wilbroad Mutafungwa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuwa hali za majeruhi zinaimarika
Akizungumzia ajali hiyo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Rombo ambaye pia ni mkuu wa wilaya hiyo Agness Hokororo amesema watu hao walikuwa wakitokea wilaya ya Rombo kwa ajili ya shughuli za chama cha Mapinduzi

Post a Comment

 
Top