Bondia
Mohamed Matumla anafanyiwa upasuaji wa kichwa muda huu baada ya ngumi
aliyopigwa kuleta madhara kwenye kichwa chake na damu kubainika kuwa
imevujia huku hali yake ikiwa nzuri
Taarifa
zilizotufikia ni kuwa Vipimo vya CT scan vimeonyesha kuvuja kwa damu na
imejikusanya sehemu moja na madaktari wanahangaikia kunusuru maisha ya
mwanamasumbwi huyo ambaye hali yake si nzuri.
Operation
ilichelewa kufanyika mapema kwa kuwa alihitajika kuongezewa damu,
"tumefanikiwa kupata damu ameshaongezewa na akitoka chumba cha upasuaji
ataongezewa damu nyingine"
Wapenzi na wadau wa ngumi kwa muda huu tumuombee DUWA mwenzetu operation yake ifanikiwe
SADICK & CO LTD ipo na mgonjwa toka aliposhuka kwenye ulingo na kusimamia matibabu yake yote
Tutaendelea kuwapa taarifa baada ya kutoka chumba cha upasuaji na hali yake itakavyokuwa inaendelea.
Promota STONE
Post a Comment