Chama cha mapinduzi CCM mkoa wa Mtwara kimelaani kitendo cha mkuu wa
mkoa huo Halima Dendego kuagiza kuvuliwa madaraka maafisa elimu wanne,
walimu wakuu 66 pamoja waratibu elimu kata katika kata zenye shule
zilizofanya vibaya na kudai kuwa kufanya hivyo sio njia sahihi ya
kufanya mkoa kufaulisha zaidi katika mitihani ya kitaifa.
Tamko hilo linakuja wakati mkuu wa mkoa huo akisubiri taarifa ya tume aliyoiunda kuchunguza kwanini mkoa umepata matokeo mabaya katika mtihani wa kujipima wa kidato cha pili ili aweze kuchukua hatua.
Akizungumza katika kikao cha kuhitimisha maadhimisho ya miaka arobaini ya kuzaliwa kwa CCM kwa kata ya Nyundo wilayani Mtwara,katibu wa CCM mkoani Mtwara Shaibu Akwilombe amesema hatua iliyochukuliwa na mkuu wa mkoa huyo ni za uonevu na hazijengi ubora wa elimu.
Aidha ametupia lawama serikali ya mkoa kushindwa kuiwezesha idara ya ukaguzi wa shule ambapo amedai kuwa wakaguzi hawana vitendea kazi.
Mkuu wa mkoa Halima Dendego kabla ya tamko hili aliwahi kusema kuwa hajawavua madaraka walimu kwa kushindwa kufaulisha bali kwa kubainika kuwa walikuwa vinara wa udanganyifu wa mitihani katika miaka ambayo walifanya vizuri.

Post a Comment