0


Waziri wa biashara viwanda na masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali  ameahidi kuondoa changamoto zote zinazowakabili wafanya biashara katika tamasha la biashara viwanda na masoko katika maonyesho ya mwaka ujao.

Waziri wa biashara viwanda na masoko Zanzibar Balozi Amina Salum Ali

Mh: amina amewataka wafanyabiashara walioshiriki katika maonesho hayo watoe changamoto zao mapema ili ziweze kufanyiwa kazi na kudhibitiwa zisijitokeze katika  maonesho ya mwakani.
Akizungumza na bahari fm Balozi Amina amesema katika maonesho ya mwakani watazifanyia kazi changamoto zote ambazo zimejitokeza katika maonesho yaliyopita pamoja na kuwepo kwa punguzo la kodi kwa washiriki ambao watahitaji kufanya biashara katika maonesho hayo.
Amesema licha ya kufanyiwa kazi changamoto hizo lakini pia katika maonesho ya mwakani wanampango wa kualika nchi mbali mbali kwa ajili ya kushiriki katika maonesho hayo.
Katika hatua nyengine Balozi Amina amezungumzia suala zima la kufanyika maonesho katika viwanja vya maisara amesema maonesho yataendelea kufanyika katika viwanja hivyo vya maisara mpaka litakapotafutwa eneo rasmini kwa ajili ya maonesho hayo.
Aidha amewataka wajasiria mali wadogo wadogo kuwa na utamaduni wa kushiriki katika maonesho ya biashara viwanda na masoko ili kuweza kupata elimu zaidi kwa wafanyabiashara wenzao.

Post a Comment

 
Top