0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Tanzania ina upungufu wa chakula katika baadhi ya maeneo na sio maeneo yote.
              
Waziri mkuu ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wakuu wa Idara na sekta mbali mbali katika mkoa wa Njombe, amesema kitendo cha baadhi ya watu kusema Tanzania ina baa la njaa si sahihi, kufanya hivyo ni kuwatia hofu wananchi na kutawapelekea watu kushindwa kuwa watulivu.

Mbali na hilo Waziri Mkuu amewataka wananchi kuwa wasikivu huku akiweka wazi kuwa katika baadhi ya hayo maeneo yenye upunguvu wa chakula, Serikali inaweza kupeleka chakula kwa kuwatumia wafanyabiashara.

Aidha kuhusiana na suala la kupanda kwa bei ya chakula katika maeneo mengi nchini, Mhe. Majaliwa amesema hali hiyo imechochewa kutokana na watu wengi kuhifadhi chakula kutokana na hofu ya hali ya hewa ya sasa jambo lililopelekea chakula kupanda bei.






Post a Comment

 
Top