MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi, amewapongeza walengwa wa mpango wa kunusuru kaya masikini shehia
ya Junguni Wilaya ya Wete, kwa kuibua miradi mbali mbali ya maendeleo na kufanikiwa
kwa kiasi kikubwa miradi hiyo.
Balozi Seif ameyaeleza
hayo, huko Junguni Gando Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, katika ziara yake
ya siku tatu kisiwani humo, kuangalia miradi mbali mbali ya maendeleo.
Amesema fedha za
miradi ya Tasaf, zinapaswa kutumiwa kikamilifu katika utekelezaji wa miradi
iliyokusudiwa, na sio kuingia mifukoni mwa wajanja na kushindwa kutekelezwa
mradi husika.
Mratib wa Tasaf
Kisiwani Pemba Mussa Saidi, amesema Tasaf Pemba ina vikundi 876 katika shehia
78, huku ikiwa na miradi nane ya matuta ya kuzuwia maji chumvi na miradi saba
ya mabwawa ya kuvunia maji ya mvua.
Amesema kitalu cha
junguni ni moja kati ya vitalu 28, vilivyomo katika mradi wa Tasaf Pemba,
ambapo kitalu kimeatika micheo 27,000 ya aina mbali mbali ikiwemo mikarafuu,
miembe, mivinje, michungwa, mikungu
huku kikitarajia kuatika miche 60 elfu.
huku kikitarajia kuatika miche 60 elfu.
Hata hivyo amesema
bado wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ucheleweshaji wa upatikanaji wa fedha
za walengwa ambao katika kipindi hiki bado miezi mitatu hawajalipwa fedha zao.
Post a Comment