SERIKALI ya Zanzibar imewataka wananchi wake kuwa wastahamilivu huku
kero zote za Muungano ambazo ni kikwazo katika kuleta maendeleo
zikipatiwa ufumbuzi haraka.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mohammed Aboud wakati akifungua kikao cha mawaziri wa pande mbili pamoja na makatibu wakuu na watendaji.
Alisema nia ya serikali zote mbili ni kuona kero zilizopo katika Muungano zinatatuliwa haraka ili wananchi wazidi kufaidi matunda ya Muungano ulioasisiwa na viongozi wakuu zaidi ya miaka 53 sasa.
Aboud alisema kufanyika kwa vikao hivyo ni muendelezo wa utekelezaji wa maagizo ya viongozi wakuu ambao wanasisitiza kupatiwa kwa ufumbuzi wa haraka wa kero za Muungano.
Mapema akizungumza katika kikao hicho, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Januari Makamba alisema hicho ni kikao cha nane tangu kuundwa kwa kamati ya pamoja ya kuzipatia ufumbuzi kero za Muungano mwaka 2008.
Alisema maagizo ya viongozi wakuu wa nchi akiwemo Rais John Magufuli na Rais Ali Mohamed Shein ni kuona kero zote zilizomo katika Muungano zinapatiwa ufumbuzi ili wananchi waweze kufaidika na matunda ya Muungano.
Makamba alisema wakati Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ukitimiza umri wa miaka 53 mafanikio makubwa yamepatikana kwa wananchi wa pande zote huku kero nyingi zilizokuwepo awali zikipatiwa ufumbuzi haraka.
Ofisa mmoja mwandamizi kutoka wizara ya fedha na mipango ya serikali ya Zanzibar alisema baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ambayo bado ni kikwazo ni suala la kodi kwa pande mbili ikiwemo uingizaji wa bidhaa. Kikao hicho kinatazamiwa kupata baraka za waziri mkuu wa Kassim Majaliwa pamoja na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.

Post a Comment