Nyumba zaidi ya 20 zimeezuliwa na upepo mkali wakati mvua ikinyesha usiku huu wa Januari 11,2017 katika manispaa ya Shinyanga.
Vyanzo vya habari vya Malunde1 blog vinasema mvua hiyo ya iliyoambatana
na upepo pia imejeruhi watu kadhaa katika kata ya Kitangiri manispaa ya
Shinyanga.
Diwani viti maalum tarafa ya Ibadakuli katika manispaa ya Shinyan Zuhura
Waziri amefika eneo hilo na kujionea uharibifu uliojitokeza kufuatia
mvua hiyo inayodaiwa kunyesha kwa muda takribani dakika 10 tu.
Diwani huyo amesema mvua hiyo mbali na kuharibu nyumba zaidi ya 20 pia
madarasa manne na ofisi ya walimu katika shule ya msingi Viwandani
zimeezuliwa.
Amewaomba wasamaria wema kufika katika eneo hilo ili kutoa msaada kwa wananchi waliothirika na mvua hiyo.
Amewaomba wasamaria wema kufika katika eneo hilo ili kutoa msaada kwa wananchi waliothirika na mvua hiyo.
Jeshi la zimamoto limefanya jitihada za kuokoa mali mbalimbali
Taarifa kamili tutawaletea hivi punde
Post a Comment