Ni waziri wa nishati na madini
Profesa Sospeter Muhongo akiongelea yaliyozungumzwa kwenye kikao cha
ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki ambao lengo lake ni kusaidia
nchi hizi kupata umeme mwingi wa uhakika na wa bei nafuu.
‘Sasa ili tuyapate hayo matatu
tunalazimika kuwa kama nchi nyingine duniani ambazo zinauziana umeme,
ndugu zangu Watanzania hadi sasa hata sisi Tanzania tunanunua umeme
kutoka Uganda karibu megawati 17, kutoka Zambia Megawati 4 na Kenya
tunanunua megawati 1‘ – Profesa Muhongo
‘Huko
tunakokwenda Afrika Mashariki ijayo na Afrika kwa ujumla tumeamua
kujenga miundombinu ya kusafirisha umeme mwingi kutoka nchi moja kwenda
nchi nyingine, sasa hivi kama mnafatilia tumeanza kujenga njia ya
kusafirisha umeme kutoka Singida kwenda Kenya ya Kilovoti 400‘ – Prof. Muhongo
‘Makusudio ya kujenga njia hizi
ya kusafirisha umeme mwingi ni kwamba muda umefika nchi za kiafrika
tuuziane umeme, badala ya kununua umeme wa bei mbaya wa mafuta hapa
Tanzania… huo umeme tunaweza tukaununua Uganda au Ethiopia, kikao chetu
hiki kilikua kinajadili miradi ambayo tulikua tunapaswa kuitekeleza‘ – Profesa Muhongo
Post a Comment