Aliyekuwa
mgombea udiwani Kata ya Katanini (CCM), Josephat Mushi (45) amehukumiwa
kifungo cha miaka mitatu jela kwa kukutwa na hatia ya kutapeli Sh30
milioni kinyume na sheria.
Wakili
wa Serikali, Lucy Kiusa amesema mshtakiwa huyo alikutwa na hatia baada
ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, kuridhishwa na ushahidi uliotolewa.
Hakimu Mfawidhi, Aidan Mwilapwa amesema mshtakiwa ana haki ya kukata rufaa endapo hajaridhika na hukumu hiyo dhidi yake.
Awali,
Wakili Kiusa amedai Novemba 4 2015, mshtakiwa alimtapeli Feruli Chua
Sh30 milioni kwa kumuuzia kiwanja chake wakati akijua alikichukulia
mkopo Benki ya Azania.
Mashahidi
wanane kutoka upande wa Jamhuri wakiongozwa na mlalamikaji aliyedai
kuwa anafahamiana na mshtakiwa kwa miaka 10 wakiwa wafanyabiashara,
amedai alinunua kiwanja hicho bila kujua kama benki iliitoa mkopo.
Chua amedai kutokana na uhusiano wake na mshtakiwa alimuamini ndipo alipoamua kuchukua uamuzi wa kununua kiwanja hicho.
Kutokana na maelezo hayo, Wakili Kiusa alimuuliza swali mshtakiwa kama alishawahi kuwa na kosa kabla.
Post a Comment