0
Mashindano ya mchezo wa bao waanza rasmi leo januari 13 yanayofanyika wilaya ya Liwale mkoani Lindi ambapo katika mashindano hayo kuna jumla ya timu 12 zinazoshiriki.

Mratibu wa mashindano hayo ndugu,Selemani Nangomwa amesema mashindano ya bao kwa mara ya pili kufanyika ikiwa lengo ni kudumisha tamaduni pamoja kuwajengea uwezo kimchezo na aliongeza kusema awamu hii kuna ongezeko kubwa la washiriki awamu hii kuna  washiriki 48 kutoka kwenye timu 12.

Timu zilizoshiriki mchezo huo wa bao katika kundi A kuna timu ya Mti Pesa,Kisimani,Namba saba,Lambai,Liwale B na RTC.

Katika kundi B kuna timu ya Majura,Nguka,Bandu,Mchenje,Kigamboni na Manyinja timu hii kwa kwa mashindano ya kwanza iliweza kuibuka na ushindi wa nafasi ya kwanza na ya pili katika mchezo wao kwenye tamasha la michezo lililofanyika desemba 31 wilayani hapa.

kwa upande wake Mohamedi Mpacha kutoka timu ya RTC alisema mchezo wa bao ni mchezo wa kufikiria haraka ili kuweza kushinda lakini katika mchezo wake aliweza kufungwa na Rashidi ngwanja katika mchezo huo wa ufunguzi aliweza kushinda hivyo mashindano hayo kwake yanamjengea uwezo wa kufikiria zao.

Nae  Emanuel Pocha moja ya mdau wa mchezo huo alisema mashindano hayo yanaenda vizuri akisema mchezo huongeza amani katika jamii.

Post a Comment

 
Top