Michuano ya
Mapinduzi Cup inatarajiwa kuendelea kutimua vumbi hii leo katika uwanja wa
Amani Visiwani Zanzibar kwa kupigwa michezo miwili majira ya saa 10:30 jioni na
saa 2:30 usiku
Mchezo wa awali
unaotarajiwa kupigwa majira ya saa 10:30 za jioni utawakutanisha mabingwa
watetezi wa michuani hiyo URA kutoka nchini Uganda dhidi ya washika bunduki wa KVZ kutokea hapa Zanzibar
Timu ya URA
inayomilikiwa na Mamlaka ya mapato
nchini Uganda walitwaa ubigwa wa kombe la mapinduzi kwa mara yao ya kwanza mwaka 2016
baada ya kumfunga mtibwa Sugar mabao 3-1
katika hatua ya fainali January 13 mwaka 2016
Kikosi cha timu ya URA kilichotwaa
ubigwa wa mapinduzi 2016
Mabao hayo ya URA
yalifungwa na Julius Ntamb na Peter Lwasa
aliyefunga magoli mawili katika dakika 85 na 88 huku bao pekee la Mtibwa na la kufutia machozi likifungwa na Jaffar
Salum na kuifanya URA kutwaa kitita cha shilingi milioni 10 za kitanzania
Mchezo huo utakaopigwa mapema hii leo utakuwa ni mchezo
wa pili kuchezwa tangu kufunguliwa rasmi kwa mashindano hayo desember 30 nna Katibu Mkuu
Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Omar Hassan King ambae
alikuwa mgeni rasmi
Mchezo wa
pili utapigwa majira ya saa 2:30 usiku kwa kuzikutanisha Simba ya Dar es Salaam
na Timu ya Taifa
Jang;ombe
ambae ndio kinara wa kundi A
Ratiba ya
michezo mengine ya Mapinduzi Cup hiyo
hapo chini
RATIBA
MAPINDUZI CUP .
1/1/2017
KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang'ombe saa 2:30 usiku.
2/1/2017
Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri,Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.
3/1/2017
Jang'ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri,KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.
4/1/2017
Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.
5/1/2017
KVZ vs Jang'ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.
6/1/2017
Taifa ya jang'ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.
7/1/2017
Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.
8/1/2017
Simba vs Jang'ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang'ombe vs URA 2:30
usiku.
10/1/2017
Saa 10: 00 nusu fainal ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainal ya pili.
13/1/2017
FAINAL saa 2: 30 usiku.
Post a Comment