0

Dar es Salaam. Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema kumekuwapo na malalamiko ya kuwa magari ya Serikali yanapendelewa na hivyo zitawekwa kamera katika barabara kuu ili kupiga picha magari yote na yenye makosa yataadhibiwa.

Kamanda Mpinga amesema hayo wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili na kusema kuwa  katika kipindi cha Januari hadi Novemba mwaka jana, makosa yaliyotokea nchini ni milioni 1.9 huku Dar es Salaam ikiwa na theluthi ya makosa hayo.

“Kamera hizo hazitajali kuwa ni gari ya Waziri, Serikali, wala Mpinga na zitapiga picha gari zote kama ilivyo kwa msemo wa kupanga ni kuchagua,” amesema.

Amesema kuwa makosa hayo yalitokana na ulevi, mwendo wa kasi, kupita katika taa nyekundu, kukatisha safari na kutokuvaa kofia ngumu.

Post a Comment

 
Top