Shirika The Mines Advisory
Group linalopinga matumizi ya mabomu yanayotegwa ardhini limesema kuwa
limetegua mabomu zaidi ya 9,000 katika miezi sita iliyopita, katika
maeneo ambayo yalikuwa yamedhibitiwa na Islamic State nchini Iraq na
Syria.
Shirika hilo linasema zinahitajika dola milioni 100 zaidi, kutegua
mabomu mengine yaliyotegwa hivi karibuni na mengine yaliyobaki kutokana
na vita za zamani.
Shirika limetoa wito huo ikiwa imetimia miaka 20 tangu hayati
Princess Diana kuzuru maeneo yaliyozikwa mabomu huko Angola ziara
iliyosaidia ulimwengu kujua kuhusu tatizo hilo.
Post a Comment