Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Rukia
Mwango Ametoa siku saba kwa wazazi wasiowapeleka watoto kufanya kabla ya hatua za kisheria hazijachukuliwa dhidi yao.
Hatua hiyo imekuba baada ya wanafunzi Zaidi ya 1600 kushindwa kuripot shule hadi sasa
Mkuu wa wilaya alisema mahudhurio
ya wanafunzi wa shule
za sekondari katika wilaya
yake ni mbaya
kwani hadi sasa wanafunzi 451
waliofika shuleni kati ya wanafunzi 2070 waliochaguliwa kujiunga
na shule za
sekondari wilayani humo
Rukia
alisema hali hiyo imetokana na
mwamko mdogo wa wazazi kuhusu elimu
na kuwahimiza watoto
kupenda shule pia sababu zinazotolewa na wazazi
hao sio za msingi
kwani wakulima walio wengi wamelipwa
fedha za mauuza ya korosho.
Mkuu
wa wilaya Alisema Kufuatia hali
hiyo ametoa muda wa siku saba kwa wazazi kuhakikisha
watoto wao wameripoti shuleni huku akiliita jambo hilo kuwa niuzembe kwa baadhi
ya wazazi hao hawathamini elimu
Post a Comment