Watafiti kutoka vyuo vikuu vya Universitat Autonoma de Barcelona na
Leidenwalichunguza ubongo wa wanawake kabla ya kushika mimba, muda mfupi
baada ya kujifungua na miaka miwili baadaye kuangalia mabadiliko kwenye
ubongo. Matokeo ya utafiti wao yamechapishwa kwenye jarida la Nature
Neuroscience.
Wanasayansi hao wanasema ujauzito hupunguza seli za ubongo katika baadhi
ya sehemu za ubongo wa mwanamke ili kumuwezesha kuhusiana vyema zaidi
na mtoto na kujiandaa kwa majukumu yake kama mama ambapo hubadilisha
ubongo wa mwanamke kwa kipindi cha hadi miaka miwili.
Uchunguzi ulifanywa kwa wanawake 25 waliokuwa wameshika mimba kwa mara
ya kwanza ulionyesha mabadiliko hayo kwenye ubongo hudumu kwa hadi miaka
miwili baada ya mwanamke kujifungua.
Watafti hao wanasema vipimo vya sehemu tofauti za ubongo hubadilika
kipindi hicho, sawa na inavyofanyika mtu anapovunja ungo, lakini hata
hivyo, hawakupata ushahidi wowote wa kuathirika kwa uwezo wa mwanamke
kuweka kumbukumbu.
Chanzo: BBC
Post a Comment