0



UPELELEZI wa kesi ya mauaji ya kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi umekamilka,anaadika Faki Sosi.
Mbele ya Thomas Simba Hakimu Mkazi Mkuu, Pamera Shinyambala wakili wa serikali amedai kuwa upelele wa kesi hiyo umekamilika hivyo ameiomba mahakama ipange tarehe kwa ajili ya kusikililiza maelezo ya mashahidi.
Miongoni mwa washtakiwa  wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Chibago Magozi (32),  John Mayunga (56),Juma Kangungu (29), Paulo Mdonondo (30), Mianda Mlewa (40), Zacharia  Msese (33), Msungwa Matonya (30) na Ahmad Kitabu (30).
Wengine ni aliyekuwa mlinzi wa marehemu Dk Mvungi, Longishu Losingo (29), dereva na mkazi wa Kitunda, Masunga Makenza (40), mkazi wa Tabata Darajani, Paulo Mdonondo (30), mkazi wa Buguruni, Zacharia Msese (33) na mkazi wa Mwananyamala, Ahmad Kitabu (30).
Kesi hiyo itaendelea tarehe 29 Disemba mwaka huu.
Inadaiwa kuwa Kwa pamoja  wanadaiwa hao Novemba 3, mwaka 2013, walifanya kosa hilo la mauaji kinyume na kifungu cha 196 cha sheria na kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Post a Comment

 
Top