Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni hiyo Rashid Shamte akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu kuingiza umeme wa upepe kwenye grid ya taifa mara baada ya
kufunguliwa kwa mkutano wa wadau mbalimbali wa umeme.
KAMPUNI
ya kuzalisha umeme wa upepo Afrika Mashariki imesema iko kwenye
mchakato wa kuingiza umeme huo kwenye gridi ya taifa, baada ya kukidhi
vigezo vya kitaifa.
Akizungumza
leo Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Rashid Shamte
alisema mradi huo unafanywa kwa ushirikiano na taasisi ya fedha ya
Kimataifa iliyochini ya benki ya dunia.
Alisema
taasisi hiyo imetoa dola za kimarekani milioni 300 kwa ajili ya
kufanikisha mradi huo mkubwa, utakaonufaisha sio tu watanzania bali nchi
nyingine.“Tutakuwa
na miradi mikubwa lakini sasa tunaelekea kuingiza upepo wa umeme kwenye
gridi ya taifa, ili tuanze kusambaza nchi nzima, watu watanufaika kwa
njia ya upepo,”alisema.
Kampuni
hiyo inatarajiwa kuwa na Kongamano la nishati mbadala litakalofahamika
kama ‘Off the Grid’ kwa ajili ya kuzungumzia namna ya kuendeleza miradi
mikubwa kwa kutumia nishati mbadala.
Alisema dhamira yao ni kuhakikisha wanakuwa na miradi mikubwa itakayofanya kazi katika nchi zilizokusini mwa jangwa la Sahara.
Post a Comment