Maafisa
wa usalama nchini Ghana wamewakamata watu watatu kwa kuhusishwa na kuwa
na ubalozi bandia wa Marekani mjini Accra ambao umetumika kuwalaghai
raia maelfu ya fedha kwa miaka 10.
Idadi
kamili ya walaghai hao haijabainika, lakini walifumaniwa na polisi wa
Ghana wakisaidiana na maafisa wa usalama wa ubalozi wa Marekani. Kwa
sasa waliokamatwa wanahojiwa ili kuelezea zaidi kuhusu udanganyifu huo.
Genge
linalosimamia ubalozi bandia liliwatafuta wateja kutoka mataifa jirani
na ndani ya nchi kisha kuwaleta kwenye jengo lililokua na bendera ya
Marekani. Kila mteja aliyekata kupata Visa ya kusafiri Marekani alitozwa
dola 6,000. Baadhi ya Visa hata hivyo zilikua halisi, hali inayozua
wasi wasi kwamba huenda walishirikiana na baadhi ya wafanyikazi wa
ubalozi wa Marekani mjini Accra.
Waliokamatwa
ni wenyeji na raia wa Uturuki.Wengi wa wateja waliodanganywa ni wakaazi
wa maeneo ya mashambani, na waliamini ubalozi huo bandia baada ya
kukutana na wanachama wa genge hilo kutoka Uturuki. Ubalozi huo bandia
pia haukuwekwa kwenye mtandao na waliwapata wateja kwa kuzungumza na
raia.
|
Post a Comment