
Timu za taifa za umri chini ya miaka 23 kwa wanaume na wanawake ambazo
hazikuwa na majina sasa zinaitwa Kilimanjaro Warriors (wanaume) wakati
wanawake ni Kilimanjaro Starlets.
Timu hizo ambazo ni maalumu kwa ajili ya michuano ya Olimpiki zitaanza
maandalizi yake Januari mwakani, na wengi wa wachezaji watakaounda timu
hizo zinazojiandaa kwa ajili ya michuano ya Olimpiki itakayofanyika
Tokyo, Japan mwaka 2020 watatoka katika timu za sasa za wachezaji wenye
umri chini ya miaka 20 (U20).
Mechi za mchujo (qualifiers) kwa ajili ya michuano ya Olimpiki ya 2020 zitaanza mapema mwaka 2019.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
Post a Comment