Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga amewatoa hofu wananchi wa
mkoa huo na kuwataka wajiandae kusherehekea sikukuu za mwisho wa mwaka
bila wasiwasi kwakuwa jeshi la polisi mkoani humo limejipanga
kukabiliana na wahalifu wanaotumia fursa ya sikukuu hizo kufanya vitendo
vinavyovunja sheria.
ACP Muliro Jumanne Muluro ameyasema hayo wakati wa mazoezi ya utayari ya
vikosi vya Jeshi la polisi mkoani Shinyanga mazoezi ambayo yanafanyika
kwa kuzunguka mitaa yote ya mji na vijiji mkoani Shinyanga kwa lengo la
kutambua maeneo korofi yanayotumiwa na wahalifu kujificha ambapo
amewataka wakazi wa mkoa wa huo kusherehekea sikuku ya Krismasi na mwaka
mpya kwa amani bila kufanya vurugu huku akitoa onyo kwa yeyote
atakayesababisha au kufanya vurugu.
Baadhi ya askari wa Jeshi la polisi mkoani shinyanga wanaoshiriki katika
mazoezi ya utayari wa kupambana na wahalifu wamedai kuwa mazoezi hayo
yanawajengea uwezo wa kutekeleza majukumu yao na hapa wanaeleza jinsi
wanavyojipanga kulinda raia na mali zao katika kipindi cha sikukuu za
mwisho wa mwaka na baada ya sikukuu kumalizika.
Post a Comment