Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam waziri wa nchi ofisi ya
rais menejimenti ya utumishi na utawala bora Angelah Kairuki amesema
licha ya matokeo ya uhakiki kufanyika kwa umakini na kuondolewa kwa kaya
55,692 zilizokuwa zinajinufaisha na mfuko wa maendeleo kwa jamii wakati
si walengwa, amemuamuru mkurugenzi mkuu wa TASAF kuwasimamisha kazi
mara moja maafisa watano walioko makao makuu wanaosimamia mpango huu
akiwemo mkurugenzi wa uratibu ambao ndio viongozi wasimamizi wakuu
pamoja na maafisa washauri na ufuatiliaji 106 walioko kwenye halmashauri
walioshindwa kufuatilia na kusimamia mpango huu na kusabaisha hasara ya
kulipwa watu wasiostahili.
Licha
ya waziri huyo kuakikishia wanahabari kuwa uhakiki umefanyika kwa
umakini na kuanzia January mwaka 2014 hadi Septemba mwaka huu zaidi ya
bilioni 6 milioni 427 kimeokolewa.
Aidha
TASAF makao makuu wametakiwa kushirikiana na halmashauri kuakikisha
wanaonufaika na fedha hizo ni walengwa tu na si vinginevyo ambapo baadhi
ya wananchi wameonyesha kupongeza hatua ya serikali kuamua kulivalia
njuga suala hilo kwani kuna baadhi ya watu waliokuwa wakijinufaisha na
TASAF wakati si walengwa.
Post a Comment