Serikali
imesema ifikapo juni tano mwakani itaendesha operesheni nchi nzima ya
kuwakamata na kuwapeleka katika vyombo vya sheria kaya ambazo
zitabainika kuwa zimeshindwa kuwa na vyoo bora kutokana na utafiti
kubaini kaya ambazo zina vyoo bora nchini ni chini ya asilimia 20.
Kwa
mujibu wa waziri wa afya, maendeleo ya jamii. jinsia, wazee na watoto
hali hiyo inatokana na takwimu kubaini kuwa ni 19 tu ya wakazi wa mijini
wana vyoo bora huku asilimia kumi tu ya wakazi wa vijijini wakitumia
vyoo bora na tayari muda wa miezi sita uliotolewa na serikali kwa kaya
zote kuwa na vyoo hivyo unazidi kwenda.
Waziri
Ummy Mwalimu ameweka msisitizo huo wakati akizindua ripoti ya matokeo
ya utafiti wa afya ya uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria na kusema
kuwa kamwe hawezi kuvumilia watanzania wakiendelea kuumwa magonjwa
yanayozuilika yakiwemo yale yanayosababishwa na ukosefu wa vyoo bora.
Naye
mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Taifa ya takwimu Dr. Albina Chuwa amesema
wamefanya utafiti huo ili kuweza kuyabaini yanayojiri katika sekta ya
afya na kuiwezesha serikali kubaini madhaifu yaliyopo sambamba na kubuni
mikakati ya kutatua changamoto hizo.