Na MALIMA LUBASHA,
MAHAKAMA
ya Wilaya ya Serengeti imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka 73
jela kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kuingia ndani ya
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuua tembo.
Hukumu hiyo ilitolewa Desemba 9 mwaka huu na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Emmanuel Ngaile wa Mahakama ya Wilaya ya Serengeti.
Alisema adhabu hiyo imetolewa kutokana na kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Waliohukumiwa
kutumikia adhabu hiyo jela ni Augen Nicodem (41) mkazi wa Mkoa wa
Kigoma, Mwita Marwa (27) na Amos Alexender (25), wote wakazi wa Wilaya
ya Serengeti.
Hakimu
Ngaile alisema katika kosa la kwanza la kuingiza na bunduki ndani ya
hifadhi kinyume cha sheria za nchi kwa ajili ya kufanyia vitendo vya
ujangili mahakama imewahukumu watumikie adhabu ya miaka 15 jela.
Alisema
kosa la pili la kusafirisha silaha kutoka Burundi hadi Tanzania
kinyume na kifungu namba 18 cha sheria ya mlipuko ya mwaka 2002 ambalo
walitiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 jela.
“Katika
kosa la tatu la kupatikana na silaha ndani ya Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti kinyume cha Sheria ya Hifadhi ya Taifa ya mwaka 2002
watatumikia kifungo cha miaka miwili kila mmoja.
“Kosa
la nne la kuingia ndani ya hifadhi bila kibali washtakiwa watumikia
kifungo cha mwaka mmoja kila mmoja na kosa la tano la kuua Tembo ndani
ya hifadhi adhabu yake ni miaka 10,” alisema.
Alisema
kwa kosa la sita la kupatikana na nyara za serikali kinyume cha sheria
ya wanyamapori namba 5 ya mwaka 2009 washtakiwa walihukumiwa kutumikia
kifungo cha miaka 30.
Post a Comment