Waziri
Mkuu wa zamani, Edward Lowassa na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif
Sharif Hamad, wamekwenda kumjulia hali Mwenyekiti wa NCCR–Mageuzi, James
Mbatia baada ya kutoka kwenye matibabu nchini India, ambako alifanyiwa
upasuaji wa mguu.
Mbatia,
ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo, alifanyiwa upasuaji huo Novemba 14
katika Hospitali ya Zydus Ahmedabad Gujarat baada ya mguu huo kumsumbua
kwa takribani miaka 37.
Lowassa
akiwa nyumbani kwa Mbatia Mbezi amesema, “Nimekuja kumuona mheshimiwa
(Mbatia). Nimefurahi zaidi baada ya kunieleza anaendelea vizuri.
Watanzania waendelee kumuombea na siku zijazo atazidi kupata nafuu
zaidi.”
Maalim Seif alimpa pole na kusema, “Binadamu ndivyo tulivyoumbwa, kuna kuumwa na usipoumwa tushukuru Mungu.”
Akizungumzia
matibabu yake, Mbatia alisema ilitumika teknolojia ya kisasa kwenye
upasuaji huo uliochukua saa nne kutokana na tatizo la mguu lililoanza
akiwa na umri wa miaka 15.
Chanzo:Mwananchi
Post a Comment