Aliyekuwa
mshambuliaji wa kalabu ya Manchester City Carlos Tevez amejiunga na
klabu ya China Shenghai Shenhua ,klabu hiyo imethibitisha.
Shenghai
wamemsajili mshambuliaji huo mwenye umri wa miaka 32, kutoka klabu ya
Boca Juniors lakini hakuna maelezo yaliotolewa kuhusu kandarasi hiyo.
Shanghai
inayofunzwa na Gus Poyet imeripotiwa kuweka kandarasi ya pauni milioni
40 ikiwemo mshahara wa zaidi ya pauni 310,000 kwa wiki.
Boca Juniors imesema: Kila la kheri Carlitos. Utakuwa myoyoni mwetu kila wakati.
Tevez alicheza kwa miaka saba katika ligi ya Uingereza na akajishindia mataji ya ligi akiwa na timu zote mbili za Manchester.
Pia
alishinda taji la vilabu bingwa Ulaya akiwa na United mwaka 2008 kabla
ya kujiunga na Juventus mwaka 2013, ambapo alijishindia mataji mawili ya
ligi ya Itali.
Mnamo tarehe 23 mwezi Disemba Chelsea iliingia
katika mkataba na Shanghai kumnununua kiungo wa kati wa Chelsea Oscar
katika uhamisho utakaogharimu pauni milioni 60.
Post a Comment