Kesi
ya ukusanyaji matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 iliyokuwa
ikiwakabili vijana saba wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
imefutwa rasmi leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es
Salaam.
Hatua
hii imekuja baada ya upande wa mashitaka kuliondoa shauri hili
mahakamani kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kifungu
cha 91(1).
Hivyo, washitakiwa wote saba wameachiwa huru na Mahakama.