Katika
kuhakikisha Watanzania wanakuwa na utaratibu wa kujihusisha na mazoezi
ili kupunguza hatari ya kupata magonjwa ambayo sio ya kuambuza, Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
imesema kuwa kampeni ya kuhamasisha mazoezi ya AFYA YAKO, MTAJI WAKO,
FANYA MAZOEZI, LINDA AFYA YAKO itakuwa endelevu na itafanyika nchi
nzima. Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati
akifunga mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari yaliyokuwa
yanalenga kutoa elimu kwa wanahabari kuhusu magonjwa yasiyo ya
kuambukiza.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kufunga mafunzo ya siku
moja kwa waNAhabari kuhusu magonjwa ambayo sio ya kuambukiza.
“Kila mwezi tutakuwa tukichagua
mkoa ambao mazoezi yatakuwa yanafanyika na yatakuwa yakiongozwa na mimi,
au naibu waziri au katibu mkuu naibu katibu mkuu au hata viongozi
wengine na hakutakuwa na gharama maana tunajua tukianza kuweka hayo
mambo kutajitokeza changamoto nyingine,” alisema Ummy. Waziri Ummy alisema alifikia uamuzi wa
kuanzisha kampeni hiyo kutokana na takwimu kuonyesha kuwepo kwa idadi
kubwa ya watu ambao wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na magonjwa
yasiyo ya kuambikiza na wakati ni jambo ambalo linaweza kumalizika kama
wananchi watabadili mfumo wao wa maisha na kuanza kuwa wanafanya
mazoezi.
Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu
akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu kampeni ya kudhibiti magonjwa
yasiyo ya kuambukiza ‘AFYA YAKO, MTAJI WAKO, FANYA MAZOEZI, LINDA AFYA
YAKO’.
“Nina mwaka hapa wizarani wakati
nimefika kipaumbele changu kilikuwa ni afya ya mama na mtoto lakini
kumbe tukasahau upande mwingine, ripoti inaonyesha kati ya watu 100
ambao wanapoteza maisha, 27 wanakufa kutokana na magonjwa yasiyo ya
kuambukiza, sasa niamua lazima tulishughulikie jambo hili,” alisema Waziri Ummy. Pia aliwataka Watanzania wote
kujitokeza Desemba, 17 katika viwanja vya Leaders Club kuanzia saa 12:30
asubuhi katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kudhibiti magonjwa
yasiyo ya kuambukiza ambapo mgeni rasmi atakuwa Makamu wa Rais, Samia
Suluhu Hassan.
Afisa
wa kitengo cha magonjwa yasiyo ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Mariam Kalomo
akiwaeleza waandishi wa habari magonjwa ambayo sio ya kuambukiza.
Mtaalamu
wa Mazoezi kutoka PAAT (Physical Activity Association of Tanzania),
Waziri Ndonde akiwafundisha waandishi wa habari aina za mazoezi na jinsi
yanavyofanyika.
Mwanahabari Majid Mjengwa akieleza jinsi ambavyo mazoezi yana umuhimu katika maisha yake ya kila siku.
Mratibu
wa Magonjwa yasiyoambukizwa wa mkoa wa Dar es Salaam, Dkt. Digna Riwa
akieleza umuhimu wa kufanya mazoezi na kula kwa kufata ushauri wa
wataalamu wa afya.
Post a Comment