0


Majira kama haya mwaka jana, Watanzania walikuwa wakijivunia kuwashuhudia nyota wao wawili wa kimataifa Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakicheza Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa vilabu, wakiwa na mabingwa wa Afrika TP-Mazembe.

SOCCER

Tayari Samatta ameshapaa na kutua Genk ya Ubeligji huku Ulimwengu akiwa hana timu baada ya mkataba wake na TP-Mazembe kumalizika.

Wikiendi hii michuano hiyo itaanza nchini Japan ambapo kuna kitu kipya kimeongezwa na shirikisho la soka duniani FIFA, ambapo sasa waamuzi wa Mechi hizo watapata msaada wa maamuzi yao kwa kutumia Video kutoka kwenye Mfumo wa Majaribio uitwao VARs, Video Assistant Referees.

SOCCER

Kwenye Mfumo huo wa Video, mwamuzi Msaidizi anakuwepo pembeni mwa Uwanja na anakuwa na Mawasiliano na Refa wa Mechi wakati wote wa Mechi hiyo akipitia Video bila kusitisha Mechi.

VARs imekuwa ikitumika kwa Majaribio huko Marekani kwenye Ligi Daraja la 3 na sasa FIFA, ikishirikiana na IFAB, ambacho ndicho chombo pekee kinachoweza kubadili Sheria za Soka, vimeafiki Majaribio hayo na sasa yameingia hatua mpya .

Mechi za Awali Desemba 11

Jeonbuk Hyundai Vs Club America

Mamelodi Sundowns Vs Kashima Antlers

Baada ya mechi hizi washindi watasonga mbele na kukutana na timu zingine kama Real Madrid katika hatua ya mtoano.

Post a Comment

 
Top