0

Je, umefanya tathimini ya mafanikio juu ya malengo yako uliyokuwa umejiwekea kwa mwaka huu 2016? Jiulize ni malengo mangapi kati ya mengi uliyokuwa umejiwekea umefanikiwa hadi sasa. Inakubidi kufanya tathimini kwa sasa ili uweze kufahamu kwa karibu ni wapi umefanikiwa na wapi hujafanikiwa na nini sababu ya kutokufanikiwa kwako hadi sasa.
Kwa kufanya hivyo itakusaidia kuelewa sababu husika zilizokufanya kushindwa kufanikiwa na hatimaye kuamua ni nini cha kufanya ili uweze kujipanga vyema kwa ajili ya mwaka unaokuja. Ukweli ni kuwa haupaswi kukata tamaa wala kukubali kukatishwa tamaa na mtu yoyote kwa namna yoyote ile kwa sababu ya kutokufanikisha malengo yako binafsi uliyokuwa umejiwekea, bali unapaswa kufahamu unayo nafasi nyingine ya kufanya marekebisho (adjustments) ili uweze kusahihisha makosa yaliyokufanya usifanikiwe katika malengo yako ya sasa na hatimaye kuweka mkakati mpya wa kufanikiwa.
Hakuna mtu duniani mwenye “guarantee” ya mafanikio ya mtu mwingine ila ni wewe ndio mwamuzi wa mafanikio yako unayoyataka katika maisha yako hadi muda huu. Kusudi la Mungu ni watu wake waishi kwa furaha na amani wakifanikiwa katika maeneo mbalimbali ya maisha yao ili wawe mfano wa kuigwa katika mazingira wanayoishi. Kubali kuwa mfano mzuri wa kuigwa dhidi ya mafanikio utakayoyapata leo kutokana na kujitoa kupanga. Usikubali kuwa masikini wala mtetezi wa umasikini huku unauwezo wa kupanga na kuondoka katika umasikini.
“A goal is a dream with a deadline.” -Napoleon Hill
Leo amua kufanya tathimini ya malengo yako kisha amua kupanga upya namna utakavyoanza safari yako ya mafanikio ndani ya mwaka 2017.
Kuna Aina nyingi za Malengo kwa kadiri mtu binafsi anavyoweza kujiwekea kulingana na uhitaji wa maeneo anayotaka kufanikiwa. Ila hapa chini nimekuwekea AINA 11 za Malengo ambayo unaweza kuchagua baadhi yake ili uweze kutumia katika kuandaa malengo yako mara kwa mara.
1: Malengo ya Biashara na Uwekezaji.
2: Malengo ya Kazi au Mahali ulipoajiriwa.
3: Malengo ya Mapato yako.
4: Malengo ya Kifedha au Mali.
5: Malengo ya Ki-Afya.
6: Malengo ya Familia.
7: Malengo ya Kujiendeleza Kifani/ Elimu/ Maarifa/ Ujuzi.
8: Malengo ya Mtandao wa Mahusiano (Networking).
9: Malengo ya Kijamii.
10: Malengo ya Ki-Tabia.
11: Malengo ya Kiroho.
NOTE: Kwa sasa sitoweza kutoa ufafanuzi juu ya malengo hayo ila ukiingia kwenye tovuti ya www.ishindotoyako.com utakutana na makala nyingi sana zinazohusiana na malengo na zinazokupa mbinu ya namna ya kuandaa malengo yako husika ili uweze kuyafanikisha. Unaweza kusoma makala hii, Aina 7 za Malengo Unayotakiwa Kujiwekea Katika Maisha Yako.
“Goals are the fuel in the furnace of achievement.” -Brian Tracy, Eat that Frog
Jifunze kupanga kabla hujaanza kufanya ili uweze kuokoa muda mwingi wakati wa utekelezaji. Mwalimu mzuri wa masuala ya mafanikio na kupanga malengo Brian Tracy kupitia kitabu chake cha Goals anasema, “Kila unapotoa muda mchache kwa ajili ya kupanga, unaokoa dakika 10 wakati wa utekelezaji.” Kwa nini leo usiamue kuchunguza kwa umakini ili ujue ni wapi unahitaji kufanikiwa katika maisha yako na kuandaa malengo yako yatakayokupa nafasi ya kufanikiwa kama unavyohitaji?
Amua kupanga ili uvute mafanikio yako karibu.

Post a Comment

 
Top