0


KAMATI ya Ushauri ya Mkoa wa Kilimanjaro imepigwa na butwaa na taarifa za wanafunzi watatu wa shule za sekondari wilayani Rombo kupewa mimba na wazazi wao wa kuwazaa.

Aidha, pamoja na mimba hizo, lakini pia baadhi ya wazazi wanaotuhumiwa katika vitendo hivyo, wamedaiwa kufanya mipango ya kutoa mimba za watoto hao ili kuficha ushahidi utakaowatia hatiani.

Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo amesema hayo wakati akichangia mada hoja kuhusu hatma ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kutokana na wimbi kubwa la kuwakatisha masomo baada ya kupewa ujauzito.

Hokororo amesema hali si ya kuridhisha wilayani mwake kwani tayari vyombo vya dola vimeanza kufuatilia tuhuma kwa baadhi ya wazazi hao ambapo mmoja wao anadaiwa kukimbilia nchini Kenya na taarifa za awali zinadaiwa huenda amejiua kwa kujinyonga.

Aliihakikishia kamati hiyo kuwa sheria itafuata mkondo wake na kwamba na hakuna mtu atakayeachwa huku uchunguzi wa kina ukifanyika kubaini iwapo aliyedaiwa kujinyonga ni mtuhumiwa ama la.

Katika taarifa ya Idara ya Elimu Mkoa, imeonesha kuwa jumla ya wanafunzi 225 wamekatishwa masomo kwa kupewa ujauzito kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Oktoba mwa huu huku wilaya za Rombo na Same zikiongoza kwa kuwa na wanafunzi 63 kwa kila wilaya.

Taarifa hiyo inaonesha wilaya zinazofuata kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaopewa ujauzito ni Mwanga yenye wanafunzi 29, Manispaa ya Moshi wanafunzi 21, Hai 19, Siha 16 na Moshi vijijini wanafunzi 14.

Kwa upande wao wadau wa elimu wa mkoa huo, Habib Msangi na Mbunge wa Viti Maalumu, Shally Raymond (CCM) wametaka serikali kupitia vyombo vya dola kuwasaka na kuchukua hatua kali kwa wale wote wanaobainika kufanya ukatili huo.

Post a Comment

 
Top