Waziri wa
Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiongea
na wauguzi hawapo pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika
jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini
lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Waziri wa
Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akikata
utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha
kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha
leo Mkoa wa Pwani.
Waziri wa
Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katikati
akiweka udongo kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo
cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani
Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Waziri wa
Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
akiangalia michoro ya jengo litakavyokua pindi litakapomalizika wakati
wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza
wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa
Pwani.
Mkuu wa
Wilaya ya Kibaha Bi. Assumpta Mshana aliyesimama akiongea na wauguzi
hawapo pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo
cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani
Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Msajili
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Lena Mfalila akiongea na wauguzi
hawapo pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la
kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo
wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Waziri wa
Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu wa tatu
kushoto akipata maelekezo kutoka kwa Msimamizi Elekezi wa mradi huo Bw.
Sauli Nkini Wa kwanza kulia kutoka Chuo Kikuu Ardhi wakati wa uwekaji wa
jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga
kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani, wa pili
kulia ni Msajili Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania Bi. Lena Mfalila.
Wenyeviti wa
Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania wakimsikiliza kwa makini Waziri wa
Afya, Maeendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo
pichani wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika jengo la kituo cha
kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha
leo Mkoa wa Pwani.
Wauguzi
mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Afya, Maeendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu hayupo pichani wakati wa uwekaji wa
jiwe la msingi katika jengo la kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga
kitaaluma nchini lililopo wilayani Kibaha leo Mkoa wa Pwani.
Habari/Picha Na Ally Daud.
Baraza la
Wauguzi na Wajunga nchini wametakiwa kutowaonea aibu wale wote
wanaoanzisha vyuo vya afya kama mradi wa kujiingizia fedha bila ya kuwa
na taaluma hiyo kwani kunapelekea kuhatarisha Maisha na afya za
watanzania.
Hayo
yamesemwa leo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati akiweka jiwe la msingi katika jengo la
kituo cha kuendeleza wauguzi na wakunga kitaaluma nchini lililopo mjini
kibaha Pwani.
“Hatusemi
wasianzishe vyuo,bali vyuo vyote viwe vyenye hadhi ya kutoa wataalam
stahili ,visajiliwe na vikaguliwe mara kwa mara ili vizalishe wauguzi
wenye sifa na ujuzi stahili,uuguzi siyo ujasiliamali,hakikisheni
mnavifungia vyuo vyote feki ili tuweze kudhibiti utitiri huu” alisema
Waziri Ummy.
Aidha Waziri
Ummy alisema hivi sasa kumekuwepo na utitiri wa vyuo vingi vya uuguzi
ambavyo havijasajiliwa na havizalishi wauguzi ambao wanastahili
kuajiriwa kwenye sekta ya afya na hivyo kuhakikisha wanasimamia taaluma
hiyo na kuvifungia mara moja vyuo vilivyokosa sifa.
Waziri Ummy
alisema kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa unaofanywa
na wauguzi katika hospitali zote nchini hivyo maboresho yatafanyika na
kuhakikisha upatikanaji wa vitendea kazi kwa wauguzi.
“Asilimia 80
za kazi zote katika hospitali zetu nchini zinafanywa na wauguzi na
wakunga hivyo Serikali imesikia kilio chenu na tutahakikisha tatizo hili
tunalitatua” alisema Ummy.
Hata hivyo
Waziri Ummy aliwataka wauguzi kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia
maadili na viapo vyao vya kitaaluma kwa maendeleo ya Afya nchini.
Kwa upande wa
Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga nchini Bi. Lena Mfalila alisema
jengo hilo linajengwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza limegharimu
pesa ya kitanzania shilingi bilioni 2.2.
Aidha Bi.
Mfalila alisema kuwa ujenzi wa kituo hicho ulianza Desemba 2015 kwa
awamu ya kwanza na kiinatarajiwa kukamililika na kuanza matumizi yake
Januari2017.
Post a Comment