0

WABUNGE wametumia nafasi ya kuchangia mjadala wa Muswada wa Huduma ya Habari wa mwaka 2016 kwa kurushiana vijembe kati ya upande wa upinzani na chama tawala badala ya kupitia vifungu kama ilivyozoeleka kwenye miswada ya sheria inayofikishwa bungeni humo.

Kitendo hicho kilimpa nguvu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba ya ‘kuwashushua’ wabunge hao alipopewa nafasi ya kuchangia ambapo alisema katika siku mbili za majadiliano ya muswada huo hakuna mbunge aliyeweka neno kwenye vifungu bali wote wamecheza siasa.

“Mkitaka kujua muswada huu ni mzuri sikilizeni kuanzia jana (juzi) hadi leo (jana) hakuna mtu aliyetia neno kwenye vifungu na kama yupo mtu asimame, wote mliamua kucheza siasa tu. Lakini kwa maana ya sheria yenyewe hakuna mtu aliyeweka neno kwa sababu kila kitu kimefanywa,” alisema.

Alisema yaliyoletwa na kambi ya upinzani yote yalikuwa yameshaondolewa na waliyoyachangia yote yalikuwa hayamo katika muswada huo.

“Awamu ya tano hatutishwi. Mwenyekiti huyu hatishwi tumeambiwa tufanye kazi tu. Kazi yetu ni kutunga sheria nawaombeni tutunge sheria, wote wameshirikishwa tofauti na mlivyosema bungeni na kama yupo mdau hakushirikishwa hakupenda mwenyewe,” alisema.

Akijitapa kufikishwa muswada huo bungeni Serukamba alisema “hili jipu lililowashinda watu kwa miaka 20 , sisi tunalitumbua leo.”

Wabunge walioonekana kurusha vijembe wakati wakichangia mjadala wa muswada huo ni pamoja na Mbunge wa Viti Maalumu Zainabu Vullu (CCM) ambaye wakati akisema muswada huo utatetea maslahi ya wanahabari alirusha kijembe kwa Mbunge wa Ubungo, Said Kubenea (Chadema) kuwa anauogopa muswada huo kwa sababu amezoea kuwalipa waandishi wake anaowaajiri kwa habari tu.

Mbunge wa Viti Maalumu, Juliana Shonza (CCM) wakati akichangia mjadala huo alipokuwa akielezea jinsi wanasiasa wanavyoingilia utendaji wa vyombo vya habari nchini aliingiliwa na Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) aliyetamka “milioni 10 hizo mlizopewa” hali iliyoonesha kumuudhi Juliana na kumweleza mbunge huyo ‘dada yangu Mdee acha bangi’.

Hata hivyo wakati Juliana anaendelea kujadili muswada huo, Mdee alisikika akisema “njoo uchukue bangi”. Mbunge wa Jang’ombe, Ally Hassan Omar King (CCM) wakati akichangia alisema wabunge wengi waliokuwa wakichangia hawakutazama kwa upande wa walaji wa habari.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top