Kwenye hali ya tofauti mchezaji Sanchez alitaka kucheza hadi mechi dhidi ya Colombia lakini kocha wa timu ya taifa alimkataza na kumwambia abaki Santiago kwa ajili ya ku-recover. Wenger akasema mchezaji huyo hatakiwi kucheza hata mechi ijayo dhidi ya Uruguay. Hivyo apande ndege arudi London.
Kocha wa Chile amepuuzia mambo hayo na Sanchez anategemewa kucheza mechi dhidi ya Uruguay siku ya Jumanne. Hali hii imeonyesha kwamba hakuna mawasiliano mazuri kati ya club ya Arsenal na timu ya taifa na wakati huo huo mchezaji wao Sanchez anataka kucheza mechi zote.
Sanchez amepigwa picha akiwa mazoezini kama kawaida na inategemewa atakua fit kucheza dhidi ya Uruguay na hatarudi London kama matakwa ya boss wake Wenger.
Post a Comment