WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Idara ya Uhamiaji imekamilisha
taratibu za kuwapatia ajira askari na maofisa 297 waliohitimu mafunzo
yao ya awali ya Uhamiaji Juni mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira ilifafanua kuwa askari na maofisa 181 walianza kupata mishahara yao Oktoba mwaka huu na waliobaki 116 watapata mishahara yao mwezi huu baada ya taratibu zote za ajira zao kukamilika.
Alisema wameshaingiza taarifa zao za kiutumishi ambazo ni vyeti vya taaluma, vyeti vya kuzaliwa, barua za ajira na fomu za kudhibiti ajira kwenye mfumo shirikishi wa taarifa za kiutumishi na mishahara ambalo ni hitaji la kisheria.
“Kukamilika kwa taratibu hizo kutawezesha watumishi wengine ambao hawakupata mshahara mwezi uliopita kupata mshahara wao mwezi huu na hivyo kufanya watumishi wote kupata mishahara yao,” ilisema taarifa hiyo ya Rwegasira.
Alisema kukamilika kwa taratibu za ajira kwa askari na maofisa 181 walioanza kulipwa mishahara yao ya Oktoba kulienda sambamba na kupatiwa barua zao za ajira.
Alifafanua kuwa taratibu za ajira kwa askari na maofisa hao 297 zilianza kufanyika Agosti mwaka huu baada ya vyombo vya ulinzi na usalama vilivyoko ndani ya wizara hiyo kupata idhini ya kuendelea na mchakato wa ajira kwa askari na maofisa waliokuwa wamehitimu mafunzo ya awali ya kijeshi kwenye vyuo mbalimbali vya majeshi chini ya wizara hiyo.
Alisema baada ya kupata idhini ya kuendelea na mchakato wa ajira, askari na maofisa hao 297 wote walipangiwa vituo vya kazi katika mikoa mbalimbali nje ya mkoa wa Dar es Salaam kulingana na mahitaji ya kila mkoa.

Post a Comment