0

Trump aendeleza harakati za uteuzi wa maafisa wakuu serikalini
Rais mteule wa Marekani Donald Trump ametangaza majina ya watu watatu wanaotarajiwa kuchukuwa nyadhifa kuu katika serikali yake mpya itakayoundwa baada ya kuapishwa rasmi tarehe 20 Januari.
 
Trump ametangaza majina hayo kwa ajili ya kuhudumu katika nafasi za mkuu wa idara ya ujasusi ya CIA, mkuu wa sheria na mshauri mkuu wa idara ya usalama wa taifa.
Seneta wa Alabama Jeff Sessions ameteuliwa kwa ajili ya nafasi ya mkuu wa sheria, mjumbe wa Kansas Mike Pompeo naye akateuliwa kwa ajili ya nafasi ya mkuu wa CIA huku jenerali mstaafu Michael Flynn akiteuliwa kwa ajili ya nafasi ya mshauri mkuu wa idara ya usalama wa taifa.
Hata hivyo baraza la seneti litatakiwa kuidhinisha uteuzi huo kwanza kabla ya wateule hao kuanza kuhudumu rasmi katika nyadhifa zao.
Viongozi hao walioteuliwa na Trump wanatarajiwa kuchukuwa nafasi za Loretta Lynch, John O. Brennan, na Susan Rice.

Post a Comment

 
Top