Donald Trump asema kati ya wahamiaji haramu milioni mbili
ama tatu watasafirishwa kutoka Marekani baada ya kuapishwa kuwa rais wa
nchi hiyo.
Katika mahojiano na kituo cha televisheni cha Marekani,CBS,
Trump amesema wahamiaji wote wenye rekodi za uhalifu, ikiwemo makundi
ya wahalifu na walanguzi wa dawa za kulevya ndio watakuwa kipaumbele
chake .
Hatma ya wahamiaji haramu milioni nane na ushee waliosalia itafahamika mara tu mpaka utakapokuwa salama.
Donald Trump ameongeza kuwa semhemu ya ukuta ambao aliahidi
kujenga kwenye mpaka baina ya nchi yake na Mexico, unaweza kuwa ni
uzio.
Post a Comment