0

Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea tena leo November 9 2016 kwa michezo miwili ya kukamilisha ratiba kuchezwa katika viwanja mbalimbali Tanzania, Simba walikuwa Sokoine Mbeya kucheza na Tanzania Prisons katika mchezo wao wa 15 wa Ligi.

Simba ambao waliingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kufungwa mchezo uliopita na African Lyon kwa goli 1-0, wamekubali kipigo cha pili cha goli 2-1 kutoka kwa Tanzania Prisons.

Katika mchezo huo Simba ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 43 kupitia kwa Jamal Mnyate, ila kipindi cha pili Prisons walikuja na mbinu mbadala zilizomfanya Victor Hangaya kupachika magoli mawili dakika ya 47 na 63.

Post a Comment

 
Top