0

SERIKALI imeanza kuajiri watumishi wapya na tayari imetoa nafasi 100 kwa Hospitali mpya ya kisasa ya Mloganzila, iliyopo Dar es Salaam.

Hospitali hiyo ambayo ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), imepewa pia nafasi zingine 200.

Rais John Magufuli alielezea suala hilo la ajira mpya, wakati akijibu swali na Anna Kwambaza wa TBC. “Ajira sasa zinaendelea. Tumetoa nafasi 100 kwa hopitali ya Mloganzila na zingine 200 zitafuata hivi karibuni. Hospitali hii itafunguliwa mwezi ujao” alisema Rais.

Hospitali ya Mloganzila ipo Kibamba wilayani Ubungo.. Rais aliongeza pia kuwa wameajiri watumishi 5,000 wa vyombo mbalimbali.

Alisema serikali iliposimamisha ajira, haina maana kwamba ajira hazitakuwepo, bali ilikuwa inakamilisha kwanza kuhakiki wafanyakazi na kubaini wafanyakazi hewa.

Alisema kazi ya kuhakiki watumishi hewa inaendelea na hadi sasa watumishi hewa 17,000 wameondolewa. Watu hao hewa walikuwa wakilipwa mishahara, posho na pensheni.

Rais alisema isingewezekana kwa serikali kuendesha kazi ya kuhakiki watumishi na wakati huo huo kuajiri watumishi wapya. Alisema watumishi hewa wameleta madhara makubwa. Alisema kuna benki moja imerudisha Sh bilioni 6.7 za watumishi hewa. Hakuitaja.

Post a Comment

 
Top